Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahqaf ayat 11 - الأحقَاف - Page - Juz 26
﴿وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَوۡ كَانَ خَيۡرٗا مَّا سَبَقُونَآ إِلَيۡهِۚ وَإِذۡ لَمۡ يَهۡتَدُواْ بِهِۦ فَسَيَقُولُونَ هَٰذَآ إِفۡكٞ قَدِيمٞ ﴾
[الأحقَاف: 11]
﴿وقال الذين كفروا للذين آمنوا لو كان خيرا ما سبقونا إليه وإذ﴾ [الأحقَاف: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wale walioukanusha unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, walisema wakiwaambia wale waliomuamini, “Lau huko kumuamini Muhammad kwa aliyokuja nayo ni kheri hamngalitutangulia kuamini.” Na kwa kuwa hawakujiongoza na hii Qur’ani wala hawakunufaika na ukweli uliyomo ndani yake, watasema, “Huu ni urongo uliopokewa kwa watu wa kale.” |