×

Na ambaye amewafyonya wazazi wake na akawaambia: Ati ndio mnanitisha kuwa nitafufuliwa, 46:17 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ahqaf ⮕ (46:17) ayat 17 in Swahili

46:17 Surah Al-Ahqaf ayat 17 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahqaf ayat 17 - الأحقَاف - Page - Juz 26

﴿وَٱلَّذِي قَالَ لِوَٰلِدَيۡهِ أُفّٖ لَّكُمَآ أَتَعِدَانِنِيٓ أَنۡ أُخۡرَجَ وَقَدۡ خَلَتِ ٱلۡقُرُونُ مِن قَبۡلِي وَهُمَا يَسۡتَغِيثَانِ ٱللَّهَ وَيۡلَكَ ءَامِنۡ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ فَيَقُولُ مَا هَٰذَآ إِلَّآ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ ﴾
[الأحقَاف: 17]

Na ambaye amewafyonya wazazi wake na akawaambia: Ati ndio mnanitisha kuwa nitafufuliwa, na hali vizazi vingi vimekwisha pita kabla yangu! Na hao wazazi humwomba msaada Mwenyezi Mungu (na humwambia mtoto wao): Ole wako! Amini! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Na yeye husema: Hayakuwa haya ila ni visa vya watu wa kale

❮ Previous Next ❯

ترجمة: والذي قال لوالديه أف لكما أتعدانني أن أخرج وقد خلت القرون من, باللغة السواحيلية

﴿والذي قال لوالديه أف لكما أتعدانني أن أخرج وقد خلت القرون من﴾ [الأحقَاف: 17]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na yule aliyesema kuwaambia wazazi wake wawili walipomlingania kwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na kuamini kuwa kuna kufufuliwa, “ Ubaya wenu! Je mnaniahidi kuwa nitatolewa kaburini mwangu nikiwa hai na hali kwamba makame ya ummah kabla yangu yashapita, na hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyefufuliwa?” Na hali wazazi wake wanamuomba Mwenyezi Mungu Amuongoze na huku wakimwambia, “Ole wako! Amini na usadiki na ufanye matendo mema, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli isiyokuwa na shaka.” Hapo awaambie, “Hayakuwa haya mnayoyasema isipokuwa ni mambo ya urongo waliyoyaandika watu wa mwanzo, yamenukuliwa kwenye vitabu vyao.”
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek