×

Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. 48:10 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Fath ⮕ (48:10) ayat 10 in Swahili

48:10 Surah Al-Fath ayat 10 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Fath ayat 10 - الفَتح - Page - Juz 26

﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ ٱللَّهَ يَدُ ٱللَّهِ فَوۡقَ أَيۡدِيهِمۡۚ فَمَن نَّكَثَ فَإِنَّمَا يَنكُثُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦۖ وَمَنۡ أَوۡفَىٰ بِمَا عَٰهَدَ عَلَيۡهُ ٱللَّهَ فَسَيُؤۡتِيهِ أَجۡرًا عَظِيمٗا ﴾
[الفَتح: 10]

Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Basi avunjaye ahadi hizi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake; na anaye tekeleza aliyo muahadi Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إن الذين يبايعونك إنما يبايعون الله يد الله فوق أيديهم فمن نكث, باللغة السواحيلية

﴿إن الذين يبايعونك إنما يبايعون الله يد الله فوق أيديهم فمن نكث﴾ [الفَتح: 10]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika ya hao wanaokupa mkono , ewe Mtume, wa ahadi ya kupigana hapo Ḥudaybiyah, wao kwa kweli wanampa mkono wa ahadi Mwenyezi Mungu na wanafanya mapatano na Yeye kwa kutaka Pepo Yake na radhi Zake. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Hivyo basi Yupo na wao anayasikia maneno yao, Anawaona mahali walipo na Anayajua mambo yao ya ndani na ya nje. Basi mwenye kuivunja ahadi yake aliyoitolea mkono, maangamivu ya jambo hilo yatamrudia mwenyewe; na atakayetekeleza ahadi aliyomuahidi Mwenyezi Mungu ya kuvumilia wakati wa mapambano na adui katika njia ya Mwenyezi Mungu na kumnusuru Nabii wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, Mwenyezi Mungu Atampa malipo mema mengi, nayo ni Pepo. Katika aya pana kuthibitisha sifa ya mkono kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inayonasibiana na Yeye, Aliyetakasika, bila kufananisha wala kueleza vile ulivyo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek