Quran with Swahili translation - Surah Al-Fath ayat 24 - الفَتح - Page - Juz 26
﴿وَهُوَ ٱلَّذِي كَفَّ أَيۡدِيَهُمۡ عَنكُمۡ وَأَيۡدِيَكُمۡ عَنۡهُم بِبَطۡنِ مَكَّةَ مِنۢ بَعۡدِ أَنۡ أَظۡفَرَكُمۡ عَلَيۡهِمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرًا ﴾
[الفَتح: 24]
﴿وهو الذي كف أيديهم عنكم وأيديكم عنهم ببطن مكة من بعد أن﴾ [الفَتح: 24]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Yeye Ndiye Aliyeizuia mikono ya washirikina isiwafikie nyinyi, na mikono yenu isiwafikie wao katika bonde la Makkah baada nyinyi kuwaweza wao wakawa chini ya mamlaka yanu. (washirikina hawa ndio wale waliotoka kuishambulia kambi ya askari wa Mtume wa Mwenyezi Mungu , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, hapo Ḥudaybiyah, Waislamu wakawakamata kisha wakawaachilia wasiwaue, na walikuwa ni kiasi cha wanaume themanini.) Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona matendo yenu, hakuna chochote kinafichamana Kwake |