Quran with Swahili translation - Surah Qaf ayat 45 - قٓ - Page - Juz 26
﴿نَّحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَقُولُونَۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِجَبَّارٖۖ فَذَكِّرۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ ﴾
[قٓ: 45]
﴿نحن أعلم بما يقولون وما أنت عليهم بجبار فذكر بالقرآن من يخاف﴾ [قٓ: 45]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sisi ni wajuzi zaidi kwa wanayoyasema hawa washirikina, ya kumzulia Mwenyezi Mungu urongo na kukanusha aya Zake. Na hukuwa wewe, ewe Mtume, umepewa nguvu juu yao ya kuwalazimisha waingie katika Uislamu, hakika ni kwamba wewe umetumilizwa uwe mfikishaji. Basi mkumbushe kwa Qur’ani anayeogopa onyo langu, kwa kuwa asiyeogopa onyo (la Mwenyezi Mungu) hafaidiki kwa kukumbushwa |