Quran with Swahili translation - Surah AT-Tur ayat 23 - الطُّور - Page - Juz 27
﴿يَتَنَٰزَعُونَ فِيهَا كَأۡسٗا لَّا لَغۡوٞ فِيهَا وَلَا تَأۡثِيمٞ ﴾
[الطُّور: 23]
﴿يتنازعون فيها كأسا لا لغو فيها ولا تأثيم﴾ [الطُّور: 23]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa starehe hizo ni kuwa wao watapeana gilasi ya pombe, mmoja wao atampa mwenzake, ili furaha yao ikamilike. Kinywaji hiki kinatafautiana na pombe ya duniani, hakimleweshi akili mwenye kukinywa, wala hakisababishi kubobokwa, wala maneno ya makosa na maasia |