Quran with Swahili translation - Surah An-Najm ayat 30 - النَّجم - Page - Juz 27
﴿ذَٰلِكَ مَبۡلَغُهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱهۡتَدَىٰ ﴾
[النَّجم: 30]
﴿ذلك مبلغهم من العلم إن ربك هو أعلم بمن ضل عن سبيله﴾ [النَّجم: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hali hiyo waliyonayo ndio upeo wa ujuzi wao na lengo lao. Hakika Mola wako Ndiye Anayemjua zaidi aliyepotoka kutoka kwenye njia ya uongofu, na Yeye ndiye Anayemjua zaidi aliyeongoka na akafuata njia ya Uislamu.. Hapa pana onyo kali kwa wenye kuasi na kukataa kukitumia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kufuata mwenendo wa Mtume Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wenye kufadhilisha matamanio ya nafsi na hadhi za ulimwenguni juu ya Akhera |