×

Surah An-Najm in Swahili

Quran Swahili ⮕ Surah Najm

Translation of the Meanings of Surah Najm in Swahili - السواحيلية

The Quran in Swahili - Surah Najm translated into Swahili, Surah An-Najm in Swahili. We provide accurate translation of Surah Najm in Swahili - السواحيلية, Verses 62 - Surah Number 53 - Page 526.

بسم الله الرحمن الرحيم

وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ (1)
Naapa kwa nyota inapo tua
مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ (2)
Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea
وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ (3)
Wala hatamki kwa matamanio
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ (4)
Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa
عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ (5)
Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu
ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَىٰ (6)
Mwenye kutua, akatulia
وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَىٰ (7)
Naye yuko juu kabisa upeo wa macho
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ (8)
Kisha akakaribia na akateremka
فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ (9)
Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi
فَأَوْحَىٰ إِلَىٰ عَبْدِهِ مَا أَوْحَىٰ (10)
Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia
مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ (11)
Moyo haukusema uwongo uliyo yaona
أَفَتُمَارُونَهُ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ (12)
Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona
وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ (13)
Na akamwona mara nyingine
عِندَ سِدْرَةِ الْمُنتَهَىٰ (14)
Penye Mkunazi wa mwisho
عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ (15)
Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa
إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ (16)
Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika
مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ (17)
Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka
لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَىٰ (18)
Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi
أَفَرَأَيْتُمُ اللَّاتَ وَالْعُزَّىٰ (19)
Je! Mmemuona Lata na Uzza
وَمَنَاةَ الثَّالِثَةَ الْأُخْرَىٰ (20)
Na Manaat, mwingine wa tatu
أَلَكُمُ الذَّكَرُ وَلَهُ الْأُنثَىٰ (21)
Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake
تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَىٰ (22)
Huo ni mgawanyo wa dhulma
إِنْ هِيَ إِلَّا أَسْمَاءٌ سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا أَنزَلَ اللَّهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَمَا تَهْوَى الْأَنفُسُ ۖ وَلَقَدْ جَاءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ الْهُدَىٰ (23)
Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi
أَمْ لِلْإِنسَانِ مَا تَمَنَّىٰ (24)
Ati mtu anakipata kila anacho kitamani
فَلِلَّهِ الْآخِرَةُ وَالْأُولَىٰ (25)
Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera
۞ وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ (26)
Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia
إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ لَيُسَمُّونَ الْمَلَائِكَةَ تَسْمِيَةَ الْأُنثَىٰ (27)
Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike
وَمَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ ۖ وَإِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا (28)
Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki
فَأَعْرِضْ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا (29)
Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia
ذَٰلِكَ مَبْلَغُهُم مِّنَ الْعِلْمِ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اهْتَدَىٰ (30)
Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka
وَلِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ أَسَاءُوا بِمَا عَمِلُوا وَيَجْزِيَ الَّذِينَ أَحْسَنُوا بِالْحُسْنَى (31)
Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema
الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ (32)
Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu
أَفَرَأَيْتَ الَّذِي تَوَلَّىٰ (33)
Je! Umemwona yule aliye geuka
وَأَعْطَىٰ قَلِيلًا وَأَكْدَىٰ (34)
Na akatoa kidogo, kisha akajizuia
أَعِندَهُ عِلْمُ الْغَيْبِ فَهُوَ يَرَىٰ (35)
Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona
أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ (36)
Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa
وَإِبْرَاهِيمَ الَّذِي وَفَّىٰ (37)
Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi
أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ (38)
Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ (39)
Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe
وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَىٰ (40)
Na kwamba vitendo vyake vitaonekana
ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاءَ الْأَوْفَىٰ (41)
Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu
وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الْمُنتَهَىٰ (42)
Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho
وَأَنَّهُ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَىٰ (43)
Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio
وَأَنَّهُ هُوَ أَمَاتَ وَأَحْيَا (44)
Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha
وَأَنَّهُ خَلَقَ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ (45)
Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike
مِن نُّطْفَةٍ إِذَا تُمْنَىٰ (46)
Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa
وَأَنَّ عَلَيْهِ النَّشْأَةَ الْأُخْرَىٰ (47)
Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine
وَأَنَّهُ هُوَ أَغْنَىٰ وَأَقْنَىٰ (48)
Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha
وَأَنَّهُ هُوَ رَبُّ الشِّعْرَىٰ (49)
Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra
وَأَنَّهُ أَهْلَكَ عَادًا الْأُولَىٰ (50)
Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza
وَثَمُودَ فَمَا أَبْقَىٰ (51)
Na Thamudi hakuwabakisha
وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا هُمْ أَظْلَمَ وَأَطْغَىٰ (52)
Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi
وَالْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَىٰ (53)
Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua
فَغَشَّاهَا مَا غَشَّىٰ (54)
Vikaifunika vilivyo funika
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ (55)
Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka
هَٰذَا نَذِيرٌ مِّنَ النُّذُرِ الْأُولَىٰ (56)
Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani
أَزِفَتِ الْآزِفَةُ (57)
Kiyama kimekaribia
لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ اللَّهِ كَاشِفَةٌ (58)
Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu
أَفَمِنْ هَٰذَا الْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ (59)
Je! Mnayastaajabia maneno haya
وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ (60)
Na mnacheka, wala hamlii
وَأَنتُمْ سَامِدُونَ (61)
Nanyi mmeghafilika
فَاسْجُدُوا لِلَّهِ وَاعْبُدُوا ۩ (62)
Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu
❮ Previous Next ❯

Surahs from Quran :

1- Fatiha2- Baqarah
3- Al Imran4- Nisa
5- Maidah6- Anam
7- Araf8- Anfal
9- Tawbah10- Yunus
11- Hud12- Yusuf
13- Raad14- Ibrahim
15- Hijr16- Nahl
17- Al Isra18- Kahf
19- Maryam20- TaHa
21- Anbiya22- Hajj
23- Muminun24- An Nur
25- Furqan26- Shuara
27- Naml28- Qasas
29- Ankabut30- Rum
31- Luqman32- Sajdah
33- Ahzab34- Saba
35- Fatir36- Yasin
37- Assaaffat38- Sad
39- Zumar40- Ghafir
41- Fussilat42- shura
43- Zukhruf44- Ad Dukhaan
45- Jathiyah46- Ahqaf
47- Muhammad48- Al Fath
49- Hujurat50- Qaf
51- zariyat52- Tur
53- Najm54- Al Qamar
55- Rahman56- Waqiah
57- Hadid58- Mujadilah
59- Al Hashr60- Mumtahina
61- Saff62- Jumuah
63- Munafiqun64- Taghabun
65- Talaq66- Tahrim
67- Mulk68- Qalam
69- Al-Haqqah70- Maarij
71- Nuh72- Jinn
73- Muzammil74- Muddathir
75- Qiyamah76- Insan
77- Mursalat78- An Naba
79- Naziat80- Abasa
81- Takwir82- Infitar
83- Mutaffifin84- Inshiqaq
85- Buruj86- Tariq
87- Al Ala88- Ghashiya
89- Fajr90- Al Balad
91- Shams92- Lail
93- Duha94- Sharh
95- Tin96- Al Alaq
97- Qadr98- Bayyinah
99- Zalzalah100- Adiyat
101- Qariah102- Takathur
103- Al Asr104- Humazah
105- Al Fil106- Quraysh
107- Maun108- Kawthar
109- Kafirun110- Nasr
111- Masad112- Ikhlas
113- Falaq114- An Nas