Quran with Swahili translation - Surah Al-hadid ayat 4 - الحدِيد - Page - Juz 27
﴿هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يَعۡلَمُ مَا يَلِجُ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا يَخۡرُجُ مِنۡهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا يَعۡرُجُ فِيهَاۖ وَهُوَ مَعَكُمۡ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ ﴾
[الحدِيد: 4]
﴿هو الذي خلق السموات والأرض في ستة أيام ثم استوى على العرش﴾ [الحدِيد: 4]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi kisha Akawa juu ya 'Arsh Yake iliyo juu ya viumbe Vyake vyote kuwa Juu kunakonasibiana na utukufu Wake. Anavijua vinavyoingia ardhini, miongoni mwa mbegu, mvua na visivyokuwa hivyo, na vinavyotoka humo miongoni mwa mimea, nafaka na matunda, na vinavyoshuka kutoka mbinguni, miongoni mwa mvua na vinginevyo, na vinvyopanda huko, miongoni mwa Malaika na matendo ( ya awaja), na Yeye , kutakasika ni Kwake, Yuko pamoja na nyinyi kwa ujuzi Wake popote mnapokuwa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona matendo yenu mnayoyafanya na Atawalipa kwayo |