Quran with Swahili translation - Surah Al-Mujadilah ayat 1 - المُجَادلة - Page - Juz 28
﴿قَدۡ سَمِعَ ٱللَّهُ قَوۡلَ ٱلَّتِي تُجَٰدِلُكَ فِي زَوۡجِهَا وَتَشۡتَكِيٓ إِلَى ٱللَّهِ وَٱللَّهُ يَسۡمَعُ تَحَاوُرَكُمَآۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعُۢ بَصِيرٌ ﴾
[المُجَادلة: 1]
﴿قد سمع الله قول التي تجادلك في زوجها وتشتكي إلى الله والله﴾ [المُجَادلة: 1]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ashasikia Mwenyezi Mungu neno la Khawalah binti ya Tha’labah anayekurudiarudia kuhusu mumewe Aws mwana wa al-Ṣāmit na kuhusu kile kilichotokea upande wake cha kufanya ẓihār nako ni kule kutamka mumewe kumwambia yeye, «wewe kwangu mimi ni kama mgongo wa mamangu», yaani katika uharamu wa kumuingilia, na huku anamnyenyekea Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amtatulie shida yake, na Mwenyezi Mungu Anayasikia maneno yenu na marudiano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msikizi wa kila neno, ni Muoni wa kila kitu, hakifichiki Kwake chochote chenye kufichika |