Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 47 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿قُلۡ أَرَءَيۡتَكُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُ ٱللَّهِ بَغۡتَةً أَوۡ جَهۡرَةً هَلۡ يُهۡلَكُ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلظَّٰلِمُونَ ﴾
[الأنعَام: 47]
﴿قل أرأيتكم إن أتاكم عذاب الله بغتة أو جهرة هل يهلك إلا﴾ [الأنعَام: 47]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Nambieni iwapo mateso ya Mwenyezi Mungu yamewashukia ghafla na hali kwamba nyinyi hamuna hisia nayo, au yakawa waziwazi yanaonekana na nyinyi mnayaangalia: Je, kwani kuna wanaoteswa isipokuwa wale watu madhalimu ambao wamekiuka mpaka kwa kuipeleka ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi mungu, Aliyetukuka, na kwa kukanusha kwao Mitume Yake?» |