Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 51 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَأَنذِرۡ بِهِ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحۡشَرُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ لَيۡسَ لَهُم مِّن دُونِهِۦ وَلِيّٞ وَلَا شَفِيعٞ لَّعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ ﴾
[الأنعَام: 51]
﴿وأنذر به الذين يخافون أن يحشروا إلى ربهم ليس لهم من دونه﴾ [الأنعَام: 51]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na watishe, ewe Mtume, kwa hii Qur’ani wale ambao wanajua kuwa wao watafufuliwa wapelekwe kwa Mola wao. Wao wanaiyamini ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kuwalipa mema wenye kufanya wema na kuwalipa maovu wenye kufanya uovu. Wao hawana, isipokuwa Mwenyezi Mungu, mtegemewa mwenye kuwanusuru wala muombezi mwenye kuwaombea mbele Yake Aliyetukuka Akawaokoa na adhabu Yake. Kwani huenda wao wakamcha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa kuyafanya maamrisho na kuyaepuka makatazo |