Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 58 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿قُل لَّوۡ أَنَّ عِندِي مَا تَسۡتَعۡجِلُونَ بِهِۦ لَقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡۗ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[الأنعَام: 58]
﴿قل لو أن عندي ما تستعجلون به لقضي الأمر بيني وبينكم والله﴾ [الأنعَام: 58]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, «Lau mimi nina mamlaka ya kuwateremshia adhabu ambayo mnaitaka kwa haraka, ningaliiteremsha kwenu, na uamuzi, baina yangu mimi na nyinyi, ungalitoka. Lakini hilo liko kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Na Yeye Anawajua zaidi madhalimu ambao wamepita mipaka yao wakawashirikisha wengine pamoja na Yeye |