Quran with Swahili translation - Surah Al-Munafiqun ayat 10 - المُنَافِقُونَ - Page - Juz 28
﴿وَأَنفِقُواْ مِن مَّا رَزَقۡنَٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوۡلَآ أَخَّرۡتَنِيٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ ﴾
[المُنَافِقُونَ: 10]
﴿وأنفقوا من ما رزقناكم من قبل أن يأتي أحدكم الموت فيقول رب﴾ [المُنَافِقُونَ: 10]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na toeni, enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, sehemu ya kile tulichowapa katika njia za kheri, mkilikimbilia hilo kabla ya kifo hakijamjia mmoja wenu na kuziona dalili zake na alama zake, na hapo aseme kwa kujuta, «Mola wangu! Si unipe muda na uahirishe kifo changu kipindi kifupi! Nipate kutoa sadaka sehemu ya mali yangu na niwe miongoni mwa watu wema wachamungu.» |