Quran with Swahili translation - Surah Al-Mulk ayat 1 - المُلك - Page - Juz 29
﴿تَبَٰرَكَ ٱلَّذِي بِيَدِهِ ٱلۡمُلۡكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ ﴾
[المُلك: 1]
﴿تبارك الذي بيده الملك وهو على كل شيء قدير﴾ [المُلك: 1]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Zimekithiri kheri za Mwenyezi Mungu na wema Wake kwa viumbe Vyake, Ambaye mkononi Mwake upo ufalme wa duniani na Akhera na mamlaka ya viwili hivyo, Anapitisha amri Yake na uamuzi Wake kwenye mamlaka Yake hayo, na Yeye kwa kila jambo ni Muweza. Faida inayopatikana katika aya hii ni kuwa inathibitisha sifa ya mkono kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, kwa namna inavyonasibiana na utukufu Wake |