Quran with Swahili translation - Surah Al-Mulk ayat 15 - المُلك - Page - Juz 29
﴿هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ ذَلُولٗا فَٱمۡشُواْ فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُواْ مِن رِّزۡقِهِۦۖ وَإِلَيۡهِ ٱلنُّشُورُ ﴾
[المُلك: 15]
﴿هو الذي جعل لكم الأرض ذلولا فامشوا في مناكبها وكلوا من رزقه﴾ [المُلك: 15]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Peke Yake Ndiye Aliyewafanyia ardhi iwe nyepesi iliyotayarishwa mpate kutulia juu yake. Basi tembeeni sehemu zake na pande zake na mle riziki ya Mwenyezi Mungu Anayowatolea humo. Na Kwake Yeye Peke Yake ndio Ufufuzi kutoka makaburini mwenu ili mhesabiwe na mlipwe. Katika hii aya pana ishara ya kuhimiza utafutaji riziki na uchumaji. Pia pana dalili kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Muabudiwa wa haki Peke Yake Asiye na mshirika, na pana dalili ya uweza Wake, kukumbusha neema Zake na kuonya kuelemea duniani |