Quran with Swahili translation - Surah Al-Mulk ayat 23 - المُلك - Page - Juz 29
﴿قُلۡ هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَكُمۡ وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَۚ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ ﴾
[المُلك: 23]
﴿قل هو الذي أنشأكم وجعل لكم السمع والأبصار والأفئدة قليلا ما تشكرون﴾ [المُلك: 23]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewapatisha nyinyi kutoka kwenye hali ya kutokuwako, na akawafanya nyinyi muwe na mashikio ili msikie kwayo, macho ili muonee na nyoyo ili muelewe kwazo. Basi ni uchache, enyi makafiri, mnavyomtekelezea shukrani Mola wenu kwa neema hizi alizowaneemesha |