Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 103 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَظَلَمُواْ بِهَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ ﴾
[الأعرَاف: 103]
﴿ثم بعثنا من بعدهم موسى بآياتنا إلى فرعون وملئه فظلموا بها فانظر﴾ [الأعرَاف: 103]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kisha tulimtuma, baada ya Mitume waliotangulia kutajwa, Mūsā mwana wa 'Imrān kwa miujiza yetu iliyo wazi aende kwa Fir'awn na watu wake, wakaikataa na kuikanusha kwa udhalimu na upinzani. Tazama kwa mazingatio, namna gani tuliwafanya na tuliwazamisha hadi wa mwisho wao, huku Mūsā na watu wake wakiona? Na huo ndio mwisho wa waharibifu |