Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 141 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَإِذۡ أَنجَيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُقَتِّلُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ ﴾
[الأعرَاف: 141]
﴿وإذ أنجيناكم من آل فرعون يسومونكم سوء العذاب يقتلون أبناءكم ويستحيون نساءكم﴾ [الأعرَاف: 141]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbukeni, enyi Wana wa Isrāīl, neema zetu kwenu tulipowaokoa na kifungo cha Fir'awn na jamaa zake na unyonge na utwevu mliokuwa nao, wa kuchinjwa watoto wenu wa kiume na kuwaacha wanawake wenu ili watumike na wadharauliwe. Na katika kupitia kwenu mateso mabaya zaidi na maovu zaidi kisha kuwaokoa ni mtihani utokao kwa Mwenyezi Mungu kwenu na neema kubwa |