Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 29 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿قُلۡ أَمَرَ رَبِّي بِٱلۡقِسۡطِۖ وَأَقِيمُواْ وُجُوهَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَٱدۡعُوهُ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَۚ كَمَا بَدَأَكُمۡ تَعُودُونَ ﴾
[الأعرَاف: 29]
﴿قل أمر ربي بالقسط وأقيموا وجوهكم عند كل مسجد وادعوه مخلصين له﴾ [الأعرَاف: 29]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Mola wangu Ameniamrisha usawa, na Amewaamrisha nyinyi mumtakasie ibada katika kila sehemu za ibada, hasa katika misikiti, na mumuombe Yeye hali ya kumtakasia utiifu na ibada, na muamini kufufuliwa baada ya kufa. Na kama Alivyowaleta kutoka kuwa hamkuwako,Yeye ni Muweza kuwarudishia uhai mara nyingine.» |