Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 28 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿وَإِذَا فَعَلُواْ فَٰحِشَةٗ قَالُواْ وَجَدۡنَا عَلَيۡهَآ ءَابَآءَنَا وَٱللَّهُ أَمَرَنَا بِهَاۗ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَأۡمُرُ بِٱلۡفَحۡشَآءِۖ أَتَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ ﴾
[الأعرَاف: 28]
﴿وإذا فعلوا فاحشة قالوا وجدنا عليها آباءنا والله أمرنا بها قل إن﴾ [الأعرَاف: 28]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na makafiri wanapofanya tendo ovu, wanajitetea kwa kusema kwamba hilo ni miongoni mwa yale waliyoyapokea kutoka kwa baba zao na kwamba hilo ni katika yale Aliyoyaamrisha Mwenyzi Mungu. Waambie, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu Hawaamrishi waja Wake vitendo vichafu na viovu. Je, mnasema, kumsingizia Mwenyezi Mungu msiyoyajua, urongo na uzushi?» |