Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 39 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿وَقَالَتۡ أُولَىٰهُمۡ لِأُخۡرَىٰهُمۡ فَمَا كَانَ لَكُمۡ عَلَيۡنَا مِن فَضۡلٖ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡسِبُونَ ﴾
[الأعرَاف: 39]
﴿وقالت أولاهم لأخراهم فما كان لكم علينا من فضل فذوقوا العذاب بما﴾ [الأعرَاف: 39]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hapo watasema wale waliofuatwa miongoni mwa viongozi na wengineo kuwaambia wafuasi wao, «Sisi na nyinyi tuko sawa katika uharibifu na upotevu na katika kufanya vitendo ambavyo ndio sababu ya kupata adhabu, kwa hivyo, nyinyi hamuna ubora juu yetu.» Mwenyezi Mungu Atawaambia wao wote, «Basi ionjeni adhabu,» yaani adhabu ya Jahanamu «kwa makosa mliyoyatenda.» |