Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 106 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَءَاخَرُونَ مُرۡجَوۡنَ لِأَمۡرِ ٱللَّهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمۡ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيۡهِمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ ﴾
[التوبَة: 106]
﴿وآخرون مرجون لأمر الله إما يعذبهم وإما يتوب عليهم والله عليم حكيم﴾ [التوبَة: 106]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa hawa waliojikalisha nyuma wakaacha kuwafuata, enyi Waumini, katika vita vya Tabūk kuna wengine walioahirishwa, ili Mwenyezi Mungu Aaamue juu yao uamuzi Atakaoutoa: ima Awaadhibu Mwenyezi Mungu au Awasamehe. Hawa ni wale waliojuta kwa yale ambayo walifanya. Nao ni Murarah mwana wa al-Rabī‘, Ka‘b mwana wa Mālik na Hilāl mwana wa Umayyaha. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa Anayestahili mateso au msamaha. Ni Mwingi wa hekima katika maneno Yake yote na vitendo Vyake |