Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 62 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمۡ لِيُرۡضُوكُمۡ وَٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥٓ أَحَقُّ أَن يُرۡضُوهُ إِن كَانُواْ مُؤۡمِنِينَ ﴾
[التوبَة: 62]
﴿يحلفون بالله لكم ليرضوكم والله ورسوله أحق أن يرضوه إن كانوا مؤمنين﴾ [التوبَة: 62]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wanafiki wanaapa viapo vya urongo na wanatoa nyudhuru za kupanga ili kuwafanya Waumini waridhike na wao. Na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanastahiki zaidi na inafaa zaidi wawaridhie kwa kuwaamini na kuwatii, iwapo kweli wao ni Waumini |