Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 116 - هُود - Page - Juz 12
﴿فَلَوۡلَا كَانَ مِنَ ٱلۡقُرُونِ مِن قَبۡلِكُمۡ أُوْلُواْ بَقِيَّةٖ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡفَسَادِ فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّنۡ أَنجَيۡنَا مِنۡهُمۡۗ وَٱتَّبَعَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مَآ أُتۡرِفُواْ فِيهِ وَكَانُواْ مُجۡرِمِينَ ﴾
[هُود: 116]
﴿فلولا كان من القرون من قبلكم أولو بقية ينهون عن الفساد في﴾ [هُود: 116]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Si ilikuwa wapatikane, miongoni mwa vizazi viliyopita kabla yenu, wasalia wa watu wazuri walio wema wanaowakataza makafiri waache ukafiri wao na kufanya uharibifu katika ardhi. Hawakupatikana katika hao isipokuwa wachache miongoni mwa walioamini na Mwenyezi Mungu akawaokoa na adhabu Yake Alipowapatiliza madhalimu. Na waliozidhulumu nafsi zao, miongoni mwa watu wa kila ummah uliopita, walifuata ladha za duniani na anasa zake walizostareheshwa, na wakawa wahalifu, wenye kudhulumu kwa kufuata kwao starehe walizokuwa nazo, ndipo adhabu ikathibiti juu yao. Katika hii aya pana mazingatio na mawaidha kwa wanaofanya maasia miongoni mwa Waislamu, kwa kuwa hawaepukani na udhalimu wa nafsi zao |