Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 20 - هُود - Page - Juz 12
﴿أُوْلَٰٓئِكَ لَمۡ يَكُونُواْ مُعۡجِزِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا كَانَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنۡ أَوۡلِيَآءَۘ يُضَٰعَفُ لَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ مَا كَانُواْ يَسۡتَطِيعُونَ ٱلسَّمۡعَ وَمَا كَانُواْ يُبۡصِرُونَ ﴾
[هُود: 20]
﴿أولئك لم يكونوا معجزين في الأرض وما كان لهم من دون الله﴾ [هُود: 20]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Makafiri hao hawakuwa ni wenye kumhepa Mwenyezi Mungu kwa kumkimbia, na hawakuwa na wasaidizi wa kuwazuia wao wasipata mateso ya Mwenyezi Mungu. Wataongezewa adhabu katika Jahanamu, kwa kuwa wao walikuwa hawawezi kuisikia Qur’ani kwa namna ya kuwafanya wanufaike au wazione alama za Mwenyezi Mungu katika ulimwengu kwa namana ya kuwafanya waongoke, kwani wao walikuwa wameshughulika na ukafiri ambao walikuwa wamedumu nao |