Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 33 - الرَّعد - Page - Juz 13
﴿أَفَمَنۡ هُوَ قَآئِمٌ عَلَىٰ كُلِّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡۗ وَجَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ قُلۡ سَمُّوهُمۡۚ أَمۡ تُنَبِّـُٔونَهُۥ بِمَا لَا يَعۡلَمُ فِي ٱلۡأَرۡضِ أَم بِظَٰهِرٖ مِّنَ ٱلۡقَوۡلِۗ بَلۡ زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ مَكۡرُهُمۡ وَصُدُّواْ عَنِ ٱلسَّبِيلِۗ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنۡ هَادٖ ﴾
[الرَّعد: 33]
﴿أفمن هو قائم على كل نفس بما كسبت وجعلوا لله شركاء قل﴾ [الرَّعد: 33]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, Yule Anayesimamia kila nafsi Akiyadhibiti yale inayoyafanya, ni mwenye haki zaidi ya kuabudiwa au ni hivi viumbe visivyojiweza? Na wao, kwa ujinga wao walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika miongoni mwa viumbe Wake wakawa wanawaabudu. Waambie, ewe Mtume, «Tajeni majina yao na sifa zao.» Na hawatapata kwenye sifa zao chochote cha kuwafanya wao wastahiki kuabudiwa. Au nyinyi mnampasha habari Mwenyezi Mungu kuwa Ana washirika katika ardhi Yake ambao Hawajui? Au mnawaita ni washirika kimaneno tu bila ya kuwa na hakika? Bali Shetani aliwapambia makafiri neno lao la ubatilifu na akawazuia njia ya Mwenyezi Mungu. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu Hakumwafikia kuongoka basi hakuna yoyote mwenye kumuongoza na kumwafikia kwenye haki na uongofu |