Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 4 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِن نُّطۡفَةٖ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٞ مُّبِينٞ ﴾
[النَّحل: 4]
﴿خلق الإنسان من نطفة فإذا هو خصيم مبين﴾ [النَّحل: 4]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Amemuumba binadamu kutokana na maji matwevu, akitahamaki ajiona ana nguvu na majivuno, na akawa mkali wa utesi na kumjadili Mola wake katika kukanusha kufufuliwa na mengineyo, kama vile kusema, «Ni nani atakayeihuisha mifupa iwapo imeoza.» Na akawa ni mwenye kumsahau Mwenyezi Mungu Aliyemuumba kutoka kwenye hali ya kutokuwako |