Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 18 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿مَّن كَانَ يُرِيدُ ٱلۡعَاجِلَةَ عَجَّلۡنَا لَهُۥ فِيهَا مَا نَشَآءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلۡنَا لَهُۥ جَهَنَّمَ يَصۡلَىٰهَا مَذۡمُومٗا مَّدۡحُورٗا ﴾
[الإسرَاء: 18]
﴿من كان يريد العاجلة عجلنا له فيها ما نشاء لمن نريد ثم﴾ [الإسرَاء: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yoyote ambaye matakwa yake ni ulimwengu huu wa sasa na akaushughulikia huo peke yake, asiiamini Akhera na asifanye matendo ya kumfaa huko, Mwenyezi Mungu Atamharakishia, hapa ulimwenguni, Anayoyataka Mwenyezi Mungu na kuyapendelea miongoni mwa yale aliyoyaandika kwenye Ubao Uliohifadhiwa (Al- Lawḥ Al-Mahfūḍ) kisha Mwenyezi Mungu Atamjaalia huko Akhera moto wa Jahanamu, atauingia akiwa ni mwenye kulaumiwa, ni mwenye kufukuzwa kwenye rehema Yake Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka. Hiyo ni kwa sababu ya kutaka kwake ulimwengu na kujishughulisha nao bila ya Akhera |