Quran with Swahili translation - Surah Maryam ayat 39 - مَريَم - Page - Juz 16
﴿وَأَنذِرۡهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡحَسۡرَةِ إِذۡ قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ وَهُمۡ فِي غَفۡلَةٖ وَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ ﴾
[مَريَم: 39]
﴿وأنذرهم يوم الحسرة إذ قضي الأمر وهم في غفلة وهم لا يؤمنون﴾ [مَريَم: 39]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na uwaonye watu, ewe Mtume, Siku ya Majuto, wakati wa hukumu kutolewa, na mauti yaletwe kama kwamba ni kondoo mzuri, achinjwe hapo na na uamuzi utolewe baina ya viumbe, na hapo watu wa Imani waende Peponi na watu wa ukafiri waende Motoni, na hali wao leo katika dunia hii wameghafilika na yale ambayo walionywa nayo, hivyo basi hawaamini wala hawafanyi matendo mema |