Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 104 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَقُولُواْ رَٰعِنَا وَقُولُواْ ٱنظُرۡنَا وَٱسۡمَعُواْۗ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 104]
﴿ياأيها الذين آمنوا لا تقولوا راعنا وقولوا انظرنا واسمعوا وللكافرين عذاب أليم﴾ [البَقَرَة: 104]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi ambao mliamini, msiseme kumwambia Mtume Muhammad, rehema na amani zimshukie, “Rā’nā.” Yaani: tupatie masikizi yako, utufahamu na utufahamishe. Sababu Mayahudi walikuwa wakisema maneno haya kumwambia Nabii, rehema na amani zimshukie, wakipotoa ndimi zao kwa neno hilo, wakikusudia kumtukana na kumnasibisha na kutoelewa. Na semeni badala yake, enyi Waumini, “Undhurnā.” Yaani: tuangalie na utuchunge. Lina maana yale-yale yanayokusudiwa. «Na msikie Kitabu cha Mola wenu mnachosomewa na mkifahamu.» Na wenye kukanusha wana adhabu yenye kuumiza |