×

Hakika wale walio leta uwongo ni kundi miongoni mwenu. Msifikiri ni shari 24:11 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nur ⮕ (24:11) ayat 11 in Swahili

24:11 Surah An-Nur ayat 11 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 11 - النور - Page - Juz 18

﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ جَآءُو بِٱلۡإِفۡكِ عُصۡبَةٞ مِّنكُمۡۚ لَا تَحۡسَبُوهُ شَرّٗا لَّكُمۖ بَلۡ هُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۚ لِكُلِّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُم مَّا ٱكۡتَسَبَ مِنَ ٱلۡإِثۡمِۚ وَٱلَّذِي تَوَلَّىٰ كِبۡرَهُۥ مِنۡهُمۡ لَهُۥ عَذَابٌ عَظِيمٞ ﴾
[النور: 11]

Hakika wale walio leta uwongo ni kundi miongoni mwenu. Msifikiri ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu. Kila mtu katika wao atapata aliyo yachuma katika madhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao, atapata adhabu kubwa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إن الذين جاءوا بالإفك عصبة منكم لا تحسبوه شرا لكم بل هو, باللغة السواحيلية

﴿إن الذين جاءوا بالإفك عصبة منكم لا تحسبوه شرا لكم بل هو﴾ [النور: 11]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kwa hakika, wale waliokuja na urongo mbaya kabisa, nao ni kumsingizia Mama wa Waumini 'Aishah, radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, kuwa amefanya kitendo kichafu, ni kikundi cha watu wanaohusiana na nyinyi, enyi kongamano la Waislamu. Msidhanie maneno yao ni shari kwenu, ilivyo ni kuwa maneno yao ni kheri kwenu, kwa kuwa yalitokamana na maneno hayo kutakaswa Mama wa Waumini na uchafu, kusafika kwake na kuukuza utajo wake, kuzipandisha daraja, kuyafuta maovu na kuwasafisha Waumini. Kila mmoja aliyouzungumza urongo huo atapata malipo ya kitendo chake cha dhambi. Na yule aliyebeba jukumu kubwa zaidi katika uzushi huo, naye ni 'Abdullāh bin Ubayy bin Salūl, kiongozi wa wanafiki, Mwenyezi Mungu Amlaani, atakuwa na adhabu kubwa huko Akhera, nayo ni kukaa milele wakati waliposikia uzushi huo, nayo nikumuepushia kile ambacho hao (wazushi) walimsngizia nacho na kusema, «Huu ni urongo waziwazi juu ya 'Aishah, radhi za Mwenyezi Mungu zimshukuie
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek