Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 30 - النور - Page - Juz 18
﴿قُل لِّلۡمُؤۡمِنِينَ يَغُضُّواْ مِنۡ أَبۡصَٰرِهِمۡ وَيَحۡفَظُواْ فُرُوجَهُمۡۚ ذَٰلِكَ أَزۡكَىٰ لَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا يَصۡنَعُونَ ﴾
[النور: 30]
﴿قل للمؤمنين يغضوا من أبصارهم ويحفظوا فروجهم ذلك أزكى لهم إن الله﴾ [النور: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Nabii, uwaambie Waumini wanaume wayainamishe macho yao kutoangalia vitu visivyohalali kwao miongoni mwa wanawake na tupu, na wazilinde tupu zao na vile Alivyovifanya haramu Mwenyezi Mungu miongoni mwa uzinifu, ulawiti, kufunua tupu na mfano wa hayo. Kufanya hivyo ni usafi zaidi kwao. Kwa hakika, Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa wanayoyafanya katika yale Anayowaamrisha na kuwakataza |