Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 82 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿وَأَصۡبَحَ ٱلَّذِينَ تَمَنَّوۡاْ مَكَانَهُۥ بِٱلۡأَمۡسِ يَقُولُونَ وَيۡكَأَنَّ ٱللَّهَ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦ وَيَقۡدِرُۖ لَوۡلَآ أَن مَّنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡنَا لَخَسَفَ بِنَاۖ وَيۡكَأَنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلۡكَٰفِرُونَ ﴾
[القَصَص: 82]
﴿وأصبح الذين تمنوا مكانه بالأمس يقولون ويكأن الله يبسط الرزق لمن يشاء﴾ [القَصَص: 82]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wale waliotamani kuwa kama yeye jana yake wakawa wanasema, wakiwa na uchungu, wenye kuzingatia na wenye kuiogopa adhabu isiwashukie, «Hakika Mwenyezi Mungu Anamkunjulia riziki Anayemtaka miongoni mwa waja Wake, na Anambania Anayemtaka miongoni mwao. Lau si Mwenyezi Mungu kutuneemesha kwa kutotuadhibu kwa tulilolisema, Angalitudidimiza sisi ardhini kama Alivyomfanya Fir’awn. Kwani hujui kwamba makafiri hawafaulu, hapa duniani wala Akhera |