Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 10 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ فَإِذَآ أُوذِيَ فِي ٱللَّهِ جَعَلَ فِتۡنَةَ ٱلنَّاسِ كَعَذَابِ ٱللَّهِۖ وَلَئِن جَآءَ نَصۡرٞ مِّن رَّبِّكَ لَيَقُولُنَّ إِنَّا كُنَّا مَعَكُمۡۚ أَوَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِأَعۡلَمَ بِمَا فِي صُدُورِ ٱلۡعَٰلَمِينَ ﴾
[العَنكبُوت: 10]
﴿ومن الناس من يقول آمنا بالله فإذا أوذي في الله جعل فتنة﴾ [العَنكبُوت: 10]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa watu, kuna anayesema, «Tumemuamini Mwenyezi Mungu.» Na afanyiwapo udhia na washirikina huwa akipapatika kutokana na mateso yao na makero yao, kama anavyopapatika kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu na asivumilie makero yake, akaritadi na akaiacha Imani yake. Na lau waja ushindi kutoka kwa Mola wako, ewe Mtume, kwa watu wenye kumuamini, watasema hawa wenye kuritadi kuiacha Imani yao, «Sisi tulikuwa pamoja na nyinyi, enyi Waumini, tukiwasaidia dhidi ya maadui wenu.» Je, si Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi kuliko yoyote wa kuyajua yaliyomo ndani ya vifua vya viumbe wake wote |