Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 151 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿سَنُلۡقِي فِي قُلُوبِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلرُّعۡبَ بِمَآ أَشۡرَكُواْ بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ سُلۡطَٰنٗاۖ وَمَأۡوَىٰهُمُ ٱلنَّارُۖ وَبِئۡسَ مَثۡوَى ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[آل عِمران: 151]
﴿سنلقي في قلوب الذين كفروا الرعب بما أشركوا بالله ما لم ينـزل﴾ [آل عِمران: 151]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Tutatia fazaa na hofu kubwa katika nyoyo za waliokufuru, kwa sababu ya kumshirikisha kwao Mwenyezi Mungu na wale wanaodaiwa kuwa ni waungu. Wao hawana dalili au hoja kuwa waungu hao wana haki ya kuabudiwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi hali yao hapa duniani ni papatiko na babaiko kwa kuwaogopa Waumini. Ama mahali pao watakaposhukia Akhera ni Moto. Na hili ni kwa sababu ya udhalimu wao na uadui wao. Na makao maovu kwao ni makao haya |