Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 39 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿فَنَادَتۡهُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَهُوَ قَآئِمٞ يُصَلِّي فِي ٱلۡمِحۡرَابِ أَنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحۡيَىٰ مُصَدِّقَۢا بِكَلِمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَسَيِّدٗا وَحَصُورٗا وَنَبِيّٗا مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ ﴾
[آل عِمران: 39]
﴿فنادته الملائكة وهو قائم يصلي في المحراب أن الله يبشرك بيحيى مصدقا﴾ [آل عِمران: 39]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hapo Malaika walimuita, naye yuko katika hali ya kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu katika mahali pake pa Swala, huku anamuomba Yeye, wakamuambia. «Mwenyezi Mungu Anakupa habari yenye kukufurahisha, nayo ni kwamba utaruzukiwa mtoto ambaye jina lake ni Yaḥyā, ambaye atalisadikisha neno la Mwenyezi Mungu, naye ni 'Īsā mwana wa Maryam, amani imshukie. Huyo Yaḥyā atakuwa ni bwana wa kaumu yake, atakuwa na cheo na daraja kubwa, atakuwa ni mwenye kujihifadhi: hatendi madhambi wala hafuati matamanio ya kudhuru na atakuwa ni Nabii miongoni mwa watu wema ambao walifikia kilele cha wema.» |