Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 54 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿وَمَكَرُواْ وَمَكَرَ ٱللَّهُۖ وَٱللَّهُ خَيۡرُ ٱلۡمَٰكِرِينَ ﴾
[آل عِمران: 54]
﴿ومكروا ومكر الله والله خير الماكرين﴾ [آل عِمران: 54]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wale waliomkanusha 'Īsā, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, walifanya vitimbi kwa kumpangia wenye kumuua. Mwenyezi Mungu akamtoa anayefanana na 'Īsā kwa mtu ambaye aliwaashiria wauaji kwake, wakamshika wakamuua na wakamsulubu wakidhani kuwa ni 'Īsā, amani imshukie. Na Mwenyezi Mungu ni bora wa wenye kufanya vitimbi. Katika haya pana kuthibitisha sifa ya makr (vitimbi) kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake na ukamilifu Wake, kwa kuwa ni vitimbi vya haki na ni katika kukabiliana na vitimbi vya wenye vitimbi |