Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 37 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقۡدِرُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ ﴾
[الرُّوم: 37]
﴿أو لم يروا أن الله يبسط الرزق لمن يشاء ويقدر إن في﴾ [الرُّوم: 37]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hawajui kwamba Mwenyezi Mungu Anamkunjulia riziki Anayemtaka kwa kumjaribu: atashukuru au atakufuru? Na (kwani hawajui kwamba Yeye) Anambania riziki Anayemtaka kwa kumjaribu: je atavumilia au atababaika? Hakika katika kukunjulia na kubania kuna alama (za utendakazi wa Mwenyezi Mungu) kwa watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na wanaojua hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema Yake |