Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 38 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿فَـَٔاتِ ذَا ٱلۡقُرۡبَىٰ حَقَّهُۥ وَٱلۡمِسۡكِينَ وَٱبۡنَ ٱلسَّبِيلِۚ ذَٰلِكَ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ يُرِيدُونَ وَجۡهَ ٱللَّهِۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ ﴾
[الرُّوم: 38]
﴿فآت ذا القربى حقه والمسكين وابن السبيل ذلك خير للذين يريدون وجه﴾ [الرُّوم: 38]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi mpe , ewe mwenye kuamini, jamaa yako wa karibu haki yake ya kuunga kizazi na sadaka na mambo mengine ya wema. Na mpe masikini na mwenye uhitaji aliyekatikiwa na njia (kwa kuishiwa na pesa akiwa safarini) Zaka na sadaka. Kwani kutoa huko ni bora kwa wale wanaoukusudia kupata radhi ya Mwenyezi Mungu kwa matendo yao mema. Na wanaofanya matendo haya na megineyo miongoni mwa matendo mema, wao ndio wenye kufaulu kupata malipo ya Mwenyezi Mungu, ndio wenye kuokoka na mateso Yake |