Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 18 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿وَجَعَلۡنَا بَيۡنَهُمۡ وَبَيۡنَ ٱلۡقُرَى ٱلَّتِي بَٰرَكۡنَا فِيهَا قُرٗى ظَٰهِرَةٗ وَقَدَّرۡنَا فِيهَا ٱلسَّيۡرَۖ سِيرُواْ فِيهَا لَيَالِيَ وَأَيَّامًا ءَامِنِينَ ﴾
[سَبإ: 18]
﴿وجعلنا بينهم وبين القرى التي باركنا فيها قرى ظاهرة وقدرنا فيها السير﴾ [سَبإ: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tulijaalia, baina ya watu wa Saba’ na hali wao wako Yaman, na ile miji tuliobarikia, nayo ni Shām, kuwe na miji iliyoshikana, aliye kwenye mji wowote kati ya hiyo huuona mji mwingine. Na tukafanya mwendo wa kutembea humo ni mwendo uliokadiriwa, kutoka nyumba hadi nyumba, bila mashaka, na tukawaambia, «Endeni kwenye miji hiyo , wakati mnapotaka wa usiku au mchana, mkiwa mko kwenye amani hamuogopi adui, njaa wala kiu |