Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 19 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿فَقَالُواْ رَبَّنَا بَٰعِدۡ بَيۡنَ أَسۡفَارِنَا وَظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فَجَعَلۡنَٰهُمۡ أَحَادِيثَ وَمَزَّقۡنَٰهُمۡ كُلَّ مُمَزَّقٍۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّكُلِّ صَبَّارٖ شَكُورٖ ﴾
[سَبإ: 19]
﴿فقالوا ربنا باعد بين أسفارنا وظلموا أنفسهم فجعلناهم أحاديث ومزقناهم كل ممزق﴾ [سَبإ: 19]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwa sababu ya kuruka mipaka kwao, walichoka na raha na amani na maisha ya neema na wakasema, «Mola wetu! Ifanye miji yetu iwe mbali mbali ili safari zetu zirefuke baina ya miji hiyo, tusipate mji ulioimarika njiani tunapokwenda.» Na wakajidhulumu nafsi zao kwa kukanusha kwao, na kwa hivyo tukawaangamiza na tukawafanya ni mazingatio na mazungumzo kwa wanaokuja baada yao, na tukawatenganisha kila namna ya kuwatenganisha, na miji yao ikawa magofu. Kwa hakika yale yaliyoikumba Saba’ ni mazingatio kwa kila mwingi wa uvimilivu juu ya shida na mambo magumu, mwingi wa kushukuru neema za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka |