Quran with Swahili translation - Surah FaTir ayat 39 - فَاطِر - Page - Juz 22
﴿هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَكُمۡ خَلَٰٓئِفَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ فَمَن كَفَرَ فَعَلَيۡهِ كُفۡرُهُۥۖ وَلَا يَزِيدُ ٱلۡكَٰفِرِينَ كُفۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ إِلَّا مَقۡتٗاۖ وَلَا يَزِيدُ ٱلۡكَٰفِرِينَ كُفۡرُهُمۡ إِلَّا خَسَارٗا ﴾
[فَاطِر: 39]
﴿هو الذي جعلكم خلائف في الأرض فمن كفر فعليه كفره ولا يزيد﴾ [فَاطِر: 39]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewafanya nyinyi, enyi watu, baadhi yenu washikilie nafasi ya wengine katika ardhi. Basi Mwenye kukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu miongoni mwenu madhara yake yatamrudia mwenyewe na ule ukafiri wake. Na hauwaongezei wakanushaji ule ukanushaji wao mbele ya Mola wao isipokuwa hasira na ghadhabu, na hakuwaongezei kule kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu isipokuwa upotevu na maangamivu |