Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 36 - الزُّمَر - Page - Juz 24
﴿أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِكَافٍ عَبۡدَهُۥۖ وَيُخَوِّفُونَكَ بِٱلَّذِينَ مِن دُونِهِۦۚ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنۡ هَادٖ ﴾
[الزُّمَر: 36]
﴿أليس الله بكاف عبده ويخوفونك بالذين من دونه ومن يضلل الله فما﴾ [الزُّمَر: 36]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, kwani Mwenyezi Mungu si Mwenye kumtosheleza mja Wake Muhammad vile vitisho vya washirikina na vitimbi vyao kuwa wao hawatamfikia kwa ubaya wowote? Ndio, Yeye Atamtosheleza katika jambo la Dini yake na dunia yake, na Atamtetea dhidi ya yoyote anayemtaka kwa ubaya. Na wao wanakutisha, ewe Mtume, na waungu wao wanaodai kuwa watakudhuru. Na yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Ameondoa msaada Wake kwake na Akamfanya apotee njia ya haki, basi huyo hana muongozi wa kumuongoza Kwake |