Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 44 - الزُّمَر - Page - Juz 24
﴿قُل لِّلَّهِ ٱلشَّفَٰعَةُ جَمِيعٗاۖ لَّهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ ثُمَّ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ ﴾
[الزُّمَر: 44]
﴿قل لله الشفاعة جميعا له ملك السموات والأرض ثم إليه ترجعون﴾ [الزُّمَر: 44]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Waambie, ewe Mtume, hao washirikina, «Ni wa Mwenyezi Mungu uombezi wote. Ni Yake Yeye mamalaka ya mbinguni na ardhini na vilivyoko baina yake. Amri yote ni ya Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na hakuna yoyote atakayeombea mbele Yake isipokuwa kwa idhini Yake. Yeye Ndiye Anayemiliki mbingu na ardhi na anayeendesha mambo yake. Lilo wajibu ni kutakwa uombezi kutoka kwa anayeumiliki na atakasiwe Yeye kwa ibada, na usitakwe kutoka kwa waungu wasiodhuru wala kunufaisha, kisha Kwake Yeye mtarudishwa baada ya kufa kwenu ili mhesabiwe na mlipwe |