×

Na wala hawakumhishimu Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki kadiri yake. Na Siku 39:67 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Az-Zumar ⮕ (39:67) ayat 67 in Swahili

39:67 Surah Az-Zumar ayat 67 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 67 - الزُّمَر - Page - Juz 24

﴿وَمَا قَدَرُواْ ٱللَّهَ حَقَّ قَدۡرِهِۦ وَٱلۡأَرۡضُ جَمِيعٗا قَبۡضَتُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَٱلسَّمَٰوَٰتُ مَطۡوِيَّٰتُۢ بِيَمِينِهِۦۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ ﴾
[الزُّمَر: 67]

Na wala hawakumhishimu Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki kadiri yake. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume. Subhanahu wa Taa'la Ametakasika na Ametukuka na hayo wanayo mshirikisha nayo

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وما قدروا الله حق قدره والأرض جميعا قبضته يوم القيامة والسموات مطويات, باللغة السواحيلية

﴿وما قدروا الله حق قدره والأرض جميعا قبضته يوم القيامة والسموات مطويات﴾ [الزُّمَر: 67]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na hawa washirikina hawakumuadhimisha Mwenyezi Mungu vile Anavyostahiki kuadhimishwa, kwa kuwa wamemuabudu asiyekuwa Yeye pamoja na Yeye miongoni mwa wale wasionufaisha wala kudhuru, wakamfanya muumbwa, pamoja na uelemevu wake, kuwa ni sawa na Muumba Mtukufu, Ambaye kotokana na uweza Wake mkubwa ni kwamba ardhi yote itakuwa iko mkononi Mwake Siku ya Kiyama, na mbingu zitakuwa zimekunjwa kwa mkono Wake wa kulia. Ametakasika Mwenyezi Mungu na kutukuka kwa kuepukana na kile wanaomshirikisha nacho hao washirikina. Katika aya hii pana dalili ya kuthibitisha kushika kwa mkono, mkono wa kulia na kukunja kwa Mwenyezi Mungu kama vile inavyolingana na haiba Yake na utukufu Wake bila kueleza Yuko vipi wala kufananisha
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek