Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 49 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُمۚ بَلِ ٱللَّهُ يُزَكِّي مَن يَشَآءُ وَلَا يُظۡلَمُونَ فَتِيلًا ﴾
[النِّسَاء: 49]
﴿ألم تر إلى الذين يزكون أنفسهم بل الله يزكي من يشاء ولا﴾ [النِّسَاء: 49]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hukujua, ewe Mtume, hali ya wale wanaojisifu wenyewe na kuyasifu matendo yao kuwa yametakasika na kuwa yako mbali na uovu? Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Peke Yake Ndiye Ambaye Anamsifu Amtakaye miongoni mwa waja Wake, kwa kuwa Yeye Ndiye Ajuwaye ukweli wa matendo yao. Na wala hawatapunguziwa chochote katika matendo yao, hata kama ni kadiri ya uzi ulio kwenye mwanya wa koko ya tende |