Quran with Swahili translation - Surah Fussilat ayat 34 - فُصِّلَت - Page - Juz 24
﴿وَلَا تَسۡتَوِي ٱلۡحَسَنَةُ وَلَا ٱلسَّيِّئَةُۚ ٱدۡفَعۡ بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ فَإِذَا ٱلَّذِي بَيۡنَكَ وَبَيۡنَهُۥ عَدَٰوَةٞ كَأَنَّهُۥ وَلِيٌّ حَمِيمٞ ﴾
[فُصِّلَت: 34]
﴿ولا تستوي الحسنة ولا السيئة ادفع بالتي هي أحسن فإذا الذي بينك﴾ [فُصِّلَت: 34]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na halilingani jema la waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakasimama imara kwenye Sheria Yake, wakawafanyia wema viumbe Vyake (hilo halilingani) na baya la waliomkanusha Yeye, wakaenda kinyume na amri Yake na wakawafanyia ubaya viumbe Vyake. Msukume, ewe Mtume, kwa msamaha wako, upole wako na hisani yako yule anayekufanyia ubaya, na upambane na ubaya wake kwako kwa kumfanyia wema. Hivyo basi yule aliyekutendea ubaya ambaye baina yako wewe na yeye kuna uadui atakuwa kama kwamba yeye ni mtu aliye jamaa yako wa karibu na mwenye huruma na wewe |