Quran with Swahili translation - Surah Az-Zukhruf ayat 57 - الزُّخرُف - Page - Juz 25
﴿۞ وَلَمَّا ضُرِبَ ٱبۡنُ مَرۡيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوۡمُكَ مِنۡهُ يَصِدُّونَ ﴾
[الزُّخرُف: 57]
﴿ولما ضرب ابن مريم مثلا إذا قومك منه يصدون﴾ [الزُّخرُف: 57]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na washirikina walipopiga mfano wa Īsā mwana wa Maryam walipomjadili Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kumhoji kuwa Wanaswara wanamuabudu, unawakuta watu wako wanainua sauti zao na kupiga kelele kwa furaha na kuterema. Napo ni pale neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka lilipoteremka (Nyinyi na vile mnavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Moto, nyinyi nyote ndani ya Moto huo mtaingia). Na washirikina wakasema, «Tumeridhika kwa waungu wetu wawe na cheo cha Īsā, Mwenyezi Mungu Akateremsha neno lake (Hakika wale ambao ilitangulia kutoka kwetu kuwa wao ni wema, hao ni wenye kuepushwa nao huo Moto). Yule anayetupwa Motoni, miongoni mwa waungu wa makafiri, ni yule aliyeridhika kuabudiwa na wao |