Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahqaf ayat 6 - الأحقَاف - Page - Juz 26
﴿وَإِذَا حُشِرَ ٱلنَّاسُ كَانُواْ لَهُمۡ أَعۡدَآءٗ وَكَانُواْ بِعِبَادَتِهِمۡ كَٰفِرِينَ ﴾
[الأحقَاف: 6]
﴿وإذا حشر الناس كانوا لهم أعداء وكانوا بعبادتهم كافرين﴾ [الأحقَاف: 6]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na pindi watu watakapokusanywa Siku ya Kiyama ili wahesabiwe na walipwe, wale waungu waliokuwa wakiwaomba duniani watakuwa ni maadui zao, wakiwalaani na kujiepusha nao na kukanusha kuwa wao walikuwa wanajua kuwa wale wanawaabudu wao |